Habari

Jeshi la polisi lapiga marufuku kuandamana kumuombea Mhe. Lissu

Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam limepiga marufuku maandamo yaliyopangwa kufanywa na Baraza la Vijana Chadema (BAVICHA) ili kumuombea Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu aliyepigwa risasi Septemba 7 mwaka huu na watu wasiojulikana.

Akizungumza na waandishi wa habari, Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu, Lazaro Mambosasa alisema yapo maeneo maalumu ya kufanya ibada hivyo ni muhimu wakayatumia hayo na si vinginevyo.

Kamanda Mambosasa alisema “Nilipokea barua ya BAVICHA wakiomba kibali cha kufanya maandamano hayo lakini nimeshawajibu kwamba hilo haliruhusiwi badala yake watumie makanisa au misikiti, kutimiza azma yao na si vinginevyo, wakitaka wanaweza hata kukesha kwenye maeneo hayo.”

“Sijapiga marufuku wao kufanya maombi hayo, ila ni vyema wakakutana kanisani au msikitini na si kufanya maandamano kama walivyoomba. Polisi ina jukumu la kulinda amani na utulivu, hivyo ikitokea jambo lolote la kuashiria uvunjifu wa amani ni jukumu lao kuzuia hilo, aliongeza Mambosasa.

Makamu Mwenyekiti wa BAVICHA, Patrick ole Sosopi awali aliongea na waandishi wa habari na kueleza azma yao ya kuwakutanisha wanachama wao mbalimbali wa imani tofauti kwa ajili ya kufanya maombezi ya kitaifa, kumuombea Mbunge huyo.

Tundu Lissu kwasasa ana patiwa matibabu Nairobi nchini Kenya katika hospitali ya Aghakhan.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents