Burudani

Jibu la Jay Moe kuhusu kolabo na Cassper Nyovest & AKA

Msanii wa muziki wa hip hop Bongo, Jay Moe amesema si kwamba ameshindwa kufanya kolabo na rapper wakali wa South Africa ambako amekuwa akienda kushoot video zake bali kuna kitu anataka kutengeneza katika muziki wake kwanza.

Rapper huyo ambaye kwa sasa anafanya vizuri na ngoma yake mpya ‘Me ana You’ ameiambia FNL ya EATV kutokana kuna kipindi alikuwa kimya kwa sasa amejikita zaidi katika kujijenga upya na baada ya hapo kolabo za rapper wakali za South Africa kama Cassper Nyovest na AKA zitafuata.

“Nilikuwa nimekaa kimya kwa muda mrefu sana, kwa hiyo siwezi kuja moja kwa moja leo nikasema nataka nifanye wimbo na AKA, Joh Makini aliweza kufanya na AKA kwa sababu kabla alikuwa ameshatoa nyimbo yeye kama Joh Makini,” amesema Jay Moe.

“Let say kesho nataka kufanya wimbo na AKA atasema (Jay Moe) alifanya nyimbo gani, ataenda ataona Me and You, ataona Pesa Madafu atasema yeah let do it,” ameongeza.

AKA ameshashirikishwa na wasanii wa Bongo kama Joh Makini katika ngoma ‘Don’t Bother’ na Diamond Platnumz katika wimbo ‘Make Me Sing’.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents