Burudani

Jibu la Joh Makini kuhusu ujio wa God Engineering

Rapper kutoka kundi la Weusi, Joh Makini amefunguka kuhusu ujio wa albamu yake ambayo imeipa jina la God Engineering.

Joh Makini anayefanya vizuri na ngoma ‘Mipaka’ amesema albamu hiyo imeshakamilika ila wanaangalia ni kwa namna gani wanaweza kuisambaza.

“Ipo tayari ni mipango tu ya jinsi gani tunaweza kuisambaza kwa wingi na ikawafikia watu wengi zaidi nchini kwa sababu kutoa albamu kwenye nchi yenye watu zaidi ya Milioni 40 kama hujajipanga vizuri albamu inaweza ikaishia kwa watu wajanja wajanja wachache wa mjini na sisi lengo ni kuwafikia watu,” Joh Makini ameiambia Bongo5.

Joh Makini si msanii kwanza kutangaza ujio albamu kwa siku za hivi karibuni, Izzo Bizness, Mwasiti, Roma na Stamina (Rostam), Moni na Country Boy (MoCo) na OMG nao pia watangaza kufanya hivyo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents