Burudani

Jibu la Squeezer iwapo anamjua Harmorapa

Msanii Mkongwe wa Bongo Flava, Squeezer amejibu iwapo anamjua Harmorapa.

Squeezer ambaye kwa sasa anafanya vizuri na ngoma yake mpya ‘Sitamani’ katika mahojiano na The Playlist ya Times Fm aliulizwa iwapo anamjua Harmorapa na kujibu;

“Nilishawahi kumuona anakimbia bastola, napenda vituko vyake kuliko muziki wake, siwezi kuelezea chochote juu ya muziki wake, let’s talk about me” amesema Squeezer.

Katika hatua nyingine amesema kuwa hawezi kufanya kiki kama njia ya kujitangaza zaidi kwani anaamini katika uwezo wake wa kimuziki.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents