Burudani

Jidenna azimiwa umeme kwenye One Africa Music Fest

By  | 

Jidenna ni miongoni mwa wasanii walioshindwa kutumbuiza katika tamasha la One Africa Music Festival mjini London wikiendi hii.

Muimbaji huyo wa Nigeria mwenye makazi nchini Marekani alikuwa mionbgoni mwa wasanii zaidi ya 17 waliotakiwa kuwasha moto jukwaani katika ukumbi wa SSE Arena Wembley akiwemo na Alikiba.

Hitmaker huyo wa Bambi, kwa bahati mbaya alishindwa kupanda jukwaani kutokana na muda kumalizika hali iliyowafanya waandaaji wa tamasha hilo kuzima umeme ukumbini hapo japo waliongeza dakika 20 zaidi kwa kumalizia show hiyo.

Baada ya kutokea tatizo hilo, Jidenna kupitia mtandao wa Twitter ameandika, “Cheers to the artists and organizers of #OneAfrica! I was supposed to perform 2night but the show was cut off as I waited backstage. I’m disappointed that London wasn’t able to see me 2night. Regardless of whose to blame, to make this our time we must be on time #OneAfrica.”

Wasanii ambao walikuwa wa mwisho kutumbuiza katika tamasha hilo walikua ni Mr Flavour na P-Square.

Loading...

Jiunge na Bongo5.com sasa

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Bongo5!

Comments