Burudani ya Michezo Live

Joh Makini afunguka kuhusiana na Lord Eyez kusainishwa na Barakah The Prince (Video)

Hatimaye Joh Makini amezungumza kuhusiana na taarifa za Lord Eyez kusainishwa kwenye label ambayo Barakah The Prince ameianzisha.

Joh amesema pamoja na kuwa Lord Eyez ni mshkaji wake mkubwa, ana uhuru wa kuchukua uamuzi anaodhani una manufaa kwake.

BONTA: BARAKAH THE PRINCE KUMSAINI LORD EYEZ NI AIBU KUBWA KWENYE HIP HOP

“Mimi Lord Eyez mbali na muziki ni mshkaji wangu sana, we are family. Hata ninavyoongea na wewe wiki moja nyuma kabla sijaenda South Africa tulikuwa wote usiku huo,” amesema Joh. “Mwisho wa siku unajua naheshimu sana maamuzi ya mtu binafsi na sipendi kuingilia. Kwa mfano siwezi kuongelea uamuzi wa yeye kusainiwa au kutosainiwa na Barakah The Prince sababu that’s him,” ameongeza.

“Naheshimu kila kitu ambacho yeye anakifanya kwasababu mwisho wa siku kila mtu ana njia yake, ana maisha yake, kila mtu ana maamuzi yake. Unajua huwezi kumuamlia mtu mzima.”

MUDA UTAONGEA IWAPO NITASHINDWA AU NITAWEZA KUMRUDISHA LORD EYEZ – BARAKAH DA PRINCE

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW