Habari

Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ apelekwa mahabusu

Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ amepelekwa mahabusu katika gereza la Ruanda baada ya Wakili wa Serikali Joseph Pande kuiomba mahakama kuzuia dhamana kutokana na usalama wa wake. Sugu amepelekwa mahabusu na Mratibu wa Chadema Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Emmanuel Masonga ambaye wana tuhuma sawa.

Hakimu Mkazi wa Mahakama Michael Mteite alikubaliana na ombi hilo ambapo aliahirisha kesi hiyo hadi Januari 19 mwaka huu.

Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ na Emmanuel Masonga wanadaiwa kutoa maneno yenye kuleta chuki baina ya wananchi na serikali katika mkutano walioufanya December 30 mwaka jana.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents