Moto Hauzimwi
TECNO Spark 2

Joti ni Noma

JotiKipaji cha msanii Joti anayeigiza katika kipindi cha Ze Comedy kinachorushwa na kituo cha luninga cha EA TV kimeonekana kuwa ni tishio hali inayopelekea kuwa patashika katika mitaa ya jiji kuanzia kwa watoto, vijana mpaka wazee, kwa wengi kupenda kuigiza kile akifanyacho msanii huyu.

Joti

 

Kipaji cha msanii Joti anayeigiza katika kipindi cha Ze Comedy kinachorushwa na kituo cha luninga cha EA TV kimeonekana kuwa ni tishio hali inayopelekea kuwa patashika katika mitaa ya jiji kuanzia kwa watoto, vijana mpaka wazee, kwa wengi kupenda kuigiza kile akifanyacho msanii huyu.

 

Misemo kama vile “nitakugeuza vocha watu wakusugue, nitakugeuza ubwabwa watu wa kupakue, nitakugeuza mti watu wa kupande, nitakugeuza nazi watu wakukune, misemo hii inaonesha ni jinsi gani kijana ameweza kuwa na ubunifu wa hali ya juu katika kazi yake kwani imekuwa ni kasheshe huko mitaani kwani washabiki kibao wanataka kutumia misemo hiyo au kuiga miondoko ya mchizi huyu.

 

Ni hali ya kawaida kukuta mtu mzima mwenye familia yake mtaani akiondoka miondoko ya kushtua kama afanyavyo msanii Joti, watoto wa shule ndio usiseme.

 

Huko mitaani kila mtu ana lake la kusema kuhusiana na msanii huyu ambapo wachache sana wanakuwa wakimuhofia kuharibu watoto wao ambao wamekuwa wakiitumia misemo yake na kuiga matendo yake, “huyu jamaa ni noma kwa kweli athari zake zimeenea sana mitaani, sasa kwa bongo inatosha ameshajitangaza vya kutosha sasa waangalie uwezekano wa kutoka na nje ya nchi huko huenda wakapata mafanikio zaidi” alisema Juma Salim Dereva Tax maneo ya stendi ya mkoa.

 

“Kwa ujumla timu nzima ya Ze Commedy ni Soo mtu wangu kwani hakuna siku ambayo utaangalia kwenye luninga wasikuvunje mbavu hasa huyu Joti anatisha ile mbaya mi ananimaliza pale anapoigiza kama mtoto au mwanafunzi mama yangu nachanika mbavu” alisema Hemed Chuwa mkaanga Chipsi maeneo ya Sinza.

 

Ni mengi yaliyosemwa na yanaendeleaa kusemwa mitaani kuhusiana na msanii huyu kama tutaamua kuyaweka basi gazeti letu litakuwa ni full Joti katika kurasa zake kwa leo inatosha.

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW