Burudani

Justine Bieber apigwa marufuku nchini China

Justine Bieber anatakiwa kusahau kabisa kutembelea nchini China.

Muimbaji huyo ambaye ni raia wa Canada amezuiwa na seriksali ya China kuigia nchini humo kutokana na kuonekana kutokuwa na nidhamu baada ya video ikimuonyesha akitembea katika madhabahu ya Yasukuni jijini Tokyo, ambayo yalijengwa na Wajapan kwa heshima ya wanajeshi wake waliouawa vitani lakini kwa nchi ya China na Korea Kusini hutazama hilo kama ishara ya watu wa Japan hawajajutia makosa yaliyotendwa na watawala wa nchi hiyo China na Japan miaka ya nyuma.

Taarifa hiyo imetolewa baada ya Wizara ya Utamaduni ya China kujibu maswali kuhusu shabiki mmoja aliyeshangaa ni kwa nini hakuna ukumbi hata mmoja ambao msanii huyo atatumbuiza katika ziara yake ya barani Asia inayotarajiwa kuanza hivi karibuni.

“Justin Bieber is a gifted singer, but he is also a controversial young foreign singer. In order to maintain order in the Chinese market and purify the Chinese performance environment, it is not suitable to bring in badly behaved entertainers,” imesema taarifa ya wizara hiyo.

“We hope that as Justin Bieber matures, he can continue to improve his own words and actions, and truly become a singer beloved by the public,” imeongeza.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents