Michezo

Kamati ya FIFA yapendekeza dakika za mchezo zipunguzwe

Kamati ya Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) imetoa pendekezo la kupunguza muda wa mchezo wa mpira wa miguu kutoka dakika 90 hadi 60.

Bodi ya kimataifa ya soka duniani inatarajia kujadili pendekezo hilo linalolenga kuondoa upotezaji muda kwa makusudi, tabia inayofanywa na wachezaji uwanjani.

Aidha waliopendekeza mpango huo wanasema kuwa mechi huchezwa kwa dakika 60 pekee kati ya 90 na muda uliosalia hutumiwa vibaya na wachezaji.

Pendekezo jingine ni wachezaji kutoruhusiwa kupiga mpira mara ya pili baada ya kipa kuupangua wakati wa penalti na iwapo penati haikupigwa inavyostahili, mchezo utasitishwa na mpira wa adhabu kutolewa.

Mapendekezo mengine ni kama kuweka saa katika uwanja ambayo italingana na ile ya refa mbali pamoja na sheria mpya itakayoruhusu mchezaji kujipigia mpira au hata kutamba na mpira wakati anapopiga mpira wa adhabu.

By Godfrey Mgallah

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents