Michezo

Kamati ya FIFA yataka Platini apigwe marufuku ya maisha ya maswala ya soka

Kamati ya maadili ya FIFA imependekeza kuwa rais aliyesimamishwa kazi wa UEFA Michel Platini apigwe marufuku ya maisha asishiriki maswala yeyote ya kandanda.

151112085912_michel_platini_640x360_rianovosti_nocredit

Wakili wake ameiambia shirikisho la habari la AFP kuwa kamati ya nidhamu ilikuwa imependekeza marufuku ya maisha kwa mteja wake kufuatia malipo ya mamilioni ya Euro.

Platini na Blatter wote wanatumikia adhabau ya marufuku ya siku 90 kufuatia uchunguzi wa malipo ya dola milioni mbili.

Wakili anayemwakilisha Platini, Thibaud d’Ales ametaja kauli hiyo kuwa inayozidi mipaka.

”Kwa hakika marufuku hii bado hata haijathibitishwa kuwa kweli ilikuwa ni ufisadi ilhali mteja wangu anapendekezwa kupigwa marufuku ya maisha?”

”Haina msingi wowote kisheria” alidai D’Ales

Wawakilishi wa rais Sepp blatter walikataa kuthibitisha kuwa walikuwa wamepokea mapendekezo sawa na hayo.

Kamati ya nidhamu ya FIFA ilipendekeza jumatatu kuwa Blatter na Platini wafunguliwe mashtaka ya ufisadi na ubadhirifu wa mali ya FIFA.

Kauli yake hata hivyo itatangazwa rasmi mwezi ujao na hadi hapo itakapotoa msimamo wake Platini hatoruhusiwa kuwania urais wa shirikisho la soka duniani FIFA.

Platini ni miongoni mwa wagombea 5 wanaotaka kumrithi rais wa shirikisho hilo Sepp Blatter katika uchaguzi unaotarajiwa kufanyika mwezi Februari mwakani.

Wakili wake anadai huenda ni njama ya kumshurutisha Platini asiwanie uongozi wa FIFA katika uchaguzi ujao.

Source: BBC

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents