Kaseja Aomba Radhi Kwa Maximo

MLINDA mlango mahiri wa klabu ya Yanga , Juma Kaseja amemwomba msamaha kocha wa Taifa Stars,Mbrazil Marcio Maximo endapo kuna kosa lolote alilolifanya walipokuwa pamoja.

MLINDA mlango mahiri wa klabu ya Yanga , Juma Kaseja amemwomba msamaha kocha wa Taifa Stars,Mbrazil Marcio Maximo endapo kuna kosa lolote alilolifanya walipokuwa pamoja.

Kwa zaidi ya mwaka mmoja sasa, Kaseja hajawahi kuitwa kwenye kikosi cha Taifa Stars chini ya Maximo na alitemwa mara baada ya mpambano kati ya Taifa Stars na Senegal kuwania kufuzu fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika nchini Ghana,ambako Stars ililala 4-0.

Kaseja aliyasema hayo mwishoni mwa wiki katika mahojiano yake yaliyorusha moja kwa moja na kituo cha televisheni cha Star cha jijini Mwanza.

Alisema yeye hajui kama kuna kosa alilolifanya ambalo lilipelekea kumuudhi kocha huyo hata kufikia uamuzi wa hatua kutomuita katika kikosi chake, lakini akakiri kuwa akiwa kama binadamu mwingine inawezekana alifanya kosa bila kujijua.

“Mimi sijui kama kuna kosa nililolifanya ambalo lilimuudhi maximo, lakini mimi ni binadamu inawezekana nilifanya bila kujielewa hivyo naomba anisamehe,”alisema Kaseja.

Yeye ana mapenzi mkubwa na Tanzania pamoja na timu ya taifa naipenda nchi yangu na nipo tayari kuichezea timu ya taifa kwa moyo wote ikiwa kocha atapata nafasi.

“Mimi ni Mtanzania ninaipenda nchi yangu ningependa kutoa mchango wangu wa hali na mali kwa timu ya taifa, nipo tayari kuichezea kwa moyo wangu wote,”alisema Kaseja.

Kaseja aliongeza kwa sasa anaendelea kufanya mazoezi kwa bidii kwa vile umri wake bado una ruhusu na pindi atakapopata nafasi ya kuitwa kwenye kikosi cha Taifa Stars anataka kuthibisha hilo kwa vitendo.

“Umri wangu bado unaniruhusu kulitumikia taifa hivyo nitaendelea kufanya mazoezi kwa bidii ili nitakapoitwa mchango wangu uonekane,”alieleza Kaseja.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents