Burudani

Kat Deluna Aongea na Clouds Fm

Yule Msanii wa Kimataifa mwenye asili ya Bermuda kutoka Marekani, mwanadada kat Deluna jana alichonga Live na clouds fm na mahojiano hayo kurushwa usiku wa saa nne na mtangazaji Adam mchomvu ambaye ndiye alikuwa zamu usiku huo pamoja na Dj steve B.

Yule Msanii wa Kimataifa mwenye asili ya Bermuda kutoka Marekani, mwanadada kat Deluna jana alichonga Live na clouds fm na mahojiano hayo kurushwa usiku wa saa nne na mtangazaji ambaye ndiye alikuwa zamu usiku huo.

Katika mahojiano hayo ambayo yaliongozwa na mtangazaji aliyejipatia umaarufu siku za karibuni bwana Arnord Kayanda ama afande Nzaboyimana mwanadada Kat Deluna alibainisha ya kuwa kesho itakuwa siku yake maalum kabisa ya kuzaliwa ambapo atatimiza miaka 21 tangu kupata uhai,hivyo ataisherehekea siku hiyo muhimu kwake akiwa Tanzania.

Pia mwanadada huyo mdogo lakini mwenye vionjo vikali katika nyimbo zake alisema safari yake ya kuja  kufanya shoo Tanzania ni ya Kwanza kwake kwenye bara la Africa hivyo ana ari na matamanio makubwa kuona ni jinsi gani watu wa huku wanavyoserebuka na pia wanavyoishi.

Akiongelea kuhusu ushindi wa Obama ambaye alitangazwa rasmi kuwa mshindi wa kiti hicho cha urais wa nchi ya Marekani bibie Kat Deluna alisema yeye amepokea ushindi huo kwa furaha na alitarajia mgombea huyo ambaye alikuwa anawakilisha chama cha Democrat angeshinda

Kushusu alivyojiandaa kuhusiana na shughuli nzima ya shoo ya Fiesta  ambayo kwa mwaka huu imepewa jina la Jirambe mwanadada huyo kutoka New York alisema yeye ni msanii wa kimataifa na amepitia kwenye college maalum za muziki hivyo swala la shoo kwake si la kubabaisha.

Msanii huyo ambaye yuko chini ya lebo ya Epic Records anatarajiwa kuwasili kesho jijini Dar-Es-Salaam, na show ya Fiesta 2008 itafanyika katika viwanja vya Leaders Jumamosi ya keshokutwa kuanzia saa moja usiku.

Bongo5 inaahidi kukupa habari zaidi kuhusiana na Jirambe Fiesta 2008 hapo kesho.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents