Habari

Kauli kuwa Obama ni mwanzilishi wa ISIS yamtokea puani Trump

Donald Trump anazidi kukipa wakati mgumu chama chake cha Republican kwa kauli zake tata.

donald-trump

Hivi karibuni mgombea huyo wa urais wa Marekani, alidai kuwa Rais Barack Obama ni mwanzilishi wa kundi la ISIS lililohusika kwenye mauaji mengi ya watu wasio na hatia.

Na sasa Trump amejaribu kujitetea kuwa kauli hiyo ilikuwa ya utani na kwamba vyombo vya habari vinapindisha kauli zake.

Ijumaa hii pia aliongea kwenye mkutano wa kampeni kuwa watu waliokuwa wakimsikiliza walijua kuwa hakuwa serious na jinsi alivyomwita Obama.

“Of course they know that. Obviously I’m being sarcastic — but not that sarcastic, to be honest with you,” alisema.

Mfanyabiashara huyo awali alitoa kauli hiyo Jumatano akidai kuwa Obama na mgombea urais wa chama cha Democratic, Hillary Clinton ni waanzilishi wa ISIS na kwamba Obama ni mtu muhimu aliyeliacha kundi hilo lifanikiwe.

“No, I meant he’s the founder of ISIS. I do. He was the most valuable player. I give him the most valuable player award. I give her, too, by the way, Hillary Clinton,” alisema kwenye mahojiano ya redio.

Mtangazaji alimtetea Obama na kudai kuwa anawachukia ISIS na amekuwa akijaribu kuwaua lakini Trump alijibu: I don’t care. He was the founder. The way he got out of Iraq, that was the founding of ISIS, OK?”

Clinton alijibu tuhuma hizo kwa kutweet: No, Barack Obama is not the founder of ISIS.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents