Kenya ni Vifijo Ushindi Wa Obama

Huku Ulimwengu mzima ukiwa umepagawishwa na Ushindi wa Rais Mteule wa nchi ya Marekani,Mh Baraka Obama, mamia kwa maelfu ya wananchi wa Kenya washangilia ushindi wa rais Mteule kwa vifijo na Nderemo Katika mitaa ya miji ya Nairobi,Naivasha Nakuru na Kisumu.

Huku Ulimwengu mzima ukiwa umepagawishwa na Ushindi wa Rais Mteule wa nchi ya Marekani,Mamia kwa maelfu ya wananchi wa Kenya washangilia ushindi wa rais Mteule kwa vifijo na Nderemo.

Habari za kuaminika kutoka jijni Nairobi na mji wa Kisumu na Nakuru zinasema sehemu kubwa ya wakazi wa Miji hiyo walifurahishwa sana na Ushindi wa Obama kiasi cha kuungana na wakazi wa Kogelo mji mdogo Magharibi mwa nchi hiyo pamoja na Jamaa na ndugu wa Obama ambaye baba Yake alizaliwa hapo.

Katika kuonyesha ni jinsi gani alivyoguswa na kwa ushindi wa Rais Mteule Mheshimiwa Baraka Obama rais wa kenya Mheshimiwa Mwai kibaki wakati akituma salamu zake za pongezi alitangaza kupitia redio taifa ya KBC kuwa Kesho siku ya Alhamisi ya tarehe 6 kuwa siku ya mapumziko.

Wakati huo huo mamia ya wananchi katika nchi nyingi za Afrika wameuchukulia ushindi wa rais mteule Mheshimiwa Baraka Obama kama ushindi wa Africa.Wakizungumza kupitia vyombo mbali mbali vya habari mamia ya wananchi kwenye mitaa mingi ya majiji ya Africa kuanzia Nairobi,mpaka Senegal wameupokea ushindi wa Obama kama ushindi kwa Waafrika wote kwa kuwa Rais huyo mteule ana asili ya kiafrika toka Kenya.

Sisi wafanyakazi  wa Bongo5 tunapenda kuwapa hongera waafrika wote na kuwaunga mkono katika kusherehekea ushindi huu wa kwanza na ki historia katika medani ya kisiasa na uongozi katika nchi ya Mrekani

 

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents