Habari

Kenya: Raila Odinga awataka wafuasi wake kususia uchaguzi wa kesho

Mgombea wa kiti cha Urais nchini Kenya kupitia muunganiko wa chama cha Nasa, Raila Odinga amewataka wafuasi wake kuususia uchaguzi unaotarajiwa kufanyika kesho (Alhamisi).

Akiongea na wafuasi wake katika mkutano mkubwa ambao umefanyika jioni hii katika bustani kubwa ya ya Nairobi inayofahamika kama Uhuru Park, Odinga amesema kuwa anawashauri Wakenya ambao wanathamini demokrasia kusali sala au kukaa nyumbani.

Odinga na chama chake cha Nasa wamesusia uchaguzi huo kutokana na kutokuwa na imani na tume ya uchaguzi wa nchi hiyo, (IEBC).

Mapema leo Jumatano Mahakama nchini humo ilishindwa kusikiliza kesi ya kusitisha kufanyika kwa uchaguzi huo siku ya kesho kutokana na baadhi ya majaji kutokuwepo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents