Burudani

Kesi ya Wema Sepetu ngoma nzito, ushahidi wakataliwa kweupe

Ushahidi wa kesi ya Wema Sepetu na wenzake wawili ya matumizi ya madawa ya kulevya aina ya bangi, umezua mvutano mzito katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salam Jumanne hii.


Wema Sepetu akitoka mahakamani na wakili wake Peter Kibatala

Upande wa washtakiwa ambao unaongozwa na wakili Peter Kibatala na Tundu Lisu, umeupinga ushahidi wa vielelezo ambavyo vimefikishwa mahakamani hapo na ofisa kutoka Ofisi ya Mkemia Mkuu kwa madai kuwa kuna baadhi ya vitu vimeonekana katika ushahidi huo ambapo mwanzoni havikutajwa.

Moja ya vitu ambavyo mawakili hao wa upande wa washtakiwa wamepinga ni kutokana na wakili wa serikali, Constantine Kakula alisema ushahidi huo upo lakini hakutamka kuwa ushahidi huo ulifungwa ndani ya bahasha. Hata hivyo wakili huyo aliondoa kauli ya kusema kuwa bahasha ndio ushahidi.

Hata hivyo Hakimu Thomas Simba ambaye anasimamia kesi hiyo, aliamuru mtoa ushahidi kuifungua bahasha hiyo lakini wakili Kibatala na Lisu waliupinga tena ushahidi huo kutokana na kuonekana karatasi yenye rangi nyekundu ndani yake kitu ambacho pia mwanzoni wakili wa serikali hakusema.

Kesi hiyo imeahirishwa na itasikilizwa tena Ijumaa ya August 18 mwaka huu.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents