Habari

Video:Khadija Mwanamboka aelezea mafanikio ya mgahawa wake wa VVK na mipango ya mwakani

Mjasiriamali na mbunifu wa mavazi nchini, Khadija Mwanamboka amesema ubunifu anaoutumia kwenye mavazi, aliuhamishia kwenye biashara yake ya mgahawa wa vyakula ‘VVK’ ndio maana mwezi huu unatimiza mwaka mmoja ukiwa na mafanikio makubwa.

4K0A5075

Khadija ameiambia Bongo5 kupitia mgahawa huo wa VVK ambacho ni kirefu cha Vitu Vya Khadija uliopo Block 41 Kinondani, jijini Dar es salaam, amesema ndani ya mwaka mmoja ameweza kuvuka matarajio ya kuwafikia wateja wengi zaidi.

“Nimeamua kuwa serious kwenye hii restaurant kwa sababu wateja wetu wamekubali huduma zetu. Mimi kama mbunifu wa mavazi kuingia kwenye sekta ya chakula haikuwa ngeni. Mimi ni mbunifu wa mavazi kwahiyo nilihamisha ule ubunifu wangu kwenye upande wa chakula,” amesema.
Basicaly hata chakula ninachouza ni chakula ambacho hata mimi nakipenda. Ni chakula ambacho mimi najua kukipika,” ameongeza.

Khadija anasema baada ya kuweza kuwafikia wateja wao wengi ndani ya mwaka mmoja, sasa wamejipanga kutoa ofa nyingi kwa wafanyakazi wa maofisini.

“Tuna plan kubwa sana ya kuboresha huduma,” anasema.

“Tunataka kuwa na ofisi ambazo zitakuwa VVK members. Kwa mfano labda kwenye ofisini kuna watu 15 wamejisajiri, watu hao watapata chakula kwa nusu ya bei, kama mfano biriani ni shilingi 10,000, wao watapata kwa shilingi 5,000 kila siku. Mungu akipenda utaratibu huu utaanza mwezi wa pili lakini kwa kipindi hiki wanaweza kuendelea kupata huduma zetu za kila siku na baadaye tutawatangania kwa kutumia mitandao yetu ya kijamii pamoja na tovuti yetu.”

Pia Khadija amesema wanatoa huduma za chakula kwenye sherehe mbalimbali pamoja na kutoa ushauri.

Tazama video hapa.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents