Khaligraph Jones na Timmy Tdat waongea kuhusu ‘Kasayole’

Wasanii kutoka nchini Kenya Khaligraph Jones na Timmy Tdat na wameongea kuhusu wimbo wao mpya ‘Kasayole’ ambao ameshirikiana.

Akiongea na Bongo5 Timmy amesema, “Kasayole tunasherehekea wapi tulipotoka. Tunataka kusema asante kwa mtaa ambao umetufanya sisi tulipo leo. Jones na mimi tulikuwa tunataka kufanya kazi pamoja na tukaingia studio na maajabu yakatokea.”

Naye Khaligraph ameongeza kwa kusema, “Wakati Timmy Tdat na mimi tulipokuwa studio unajua kua ngoma inaenda kuwa moto. Kufanya kazi na wewe Kufanya kazi na yeye ni kusherehekea mitaani kwetu ilikuwa ni uzoefu mkubwa na ninatarajia kufanya kazi naye zaidi.

Wimbo huo umetayarishwa na Magix Enga, wakati huo huo video imeongozwa na Enos Olik. Tazama video hiyo hapa chini.

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW