Michezo

Kikosi cha timu ya riadha kutua nchini kesho

Timu ya taifa ya mchezo wa riadha inatarajia kuwasili hapo kesho ikitokea nchini Uingereza ilipokuwa imekwenda katika mashindano ya Dunia.

Timu hiyo yenye jumla ya wachezaji nane ilikuwa jijini London katika michuano mikubwa ya riadha ambapo mtanzania, Alphonce Simbu alitwaa medali ya shaba baada ya kushika nafasi ya tatu katika mbio ndefu.

Timu hiyo inatarajiwa kupokelewa katika uwanja wa ndenge wa JK Nyerere Jijini Dar es Salaam na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harison Mwakyembe, Mkurugenzi Mtendaji wa Multichoice Tanzania, Maharage Chande pamoja na maafisa mbalimbali waandamizi wa serikali na Vyama vya michezo.

Huku mshindi wa medali ya Shaba katika mashindano hayo Alphonce Simbu  akipata fursa ya kuonyesha rasmi medali yake hiyo kwa watanzania.

By Hamza Fumo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents