Burudani

Kilichojiri Kesi ya Lulu Mahakamani leo. Maelezo ya ushahidi wa mke wa Dkt Slaa wasomwa

Kesi ya Elizabeth ‘Lulu’ Michael inayomkabili ya kumuuwa muigizaji mwenzake Steven Kanumba bila kukusudia imeendelea kusikilzwa tena Jumatano hii katika Mahakama Kuu.

Katika kesi hiyo leo ilikuwa ni siku ya kusomwa kwa maelezo ya ushahidi uliowahi kundikwa na mke wa Dr Slaa ambaye pia alikua daktari wa Marehemu Kanumba, Josephine Mshumbisi ambaye alishindwa kufika mahakamani hapo siku ya jana kutokana na kutokuwepo nchini.

Melezo hayo yalisomwa mahakamani hapo na Polisi Detective Sergeant Nengea ambaye ndio alisaini maelezo ya ushahidi huo. Akisoma maelezo hayo ya Daktari Mshumbisi polisi Nengea amesema, Mmoja ya wateja wangu marehemu Steven Kanumba kwa mara ya kwanza alikuja kwangu mwaka 2011 kwa ajili ya kutoa sumu mwilini.

Maelezo hayo yameendelea kusema kuwa, Marehemu alikua na matatizo ya damu, upungufu wa hewa kwenye ubongo na alikuwa anasikia maumivu katika ubongo na akili kuchoka.

Wakati huo huo Jaji ambaye anasikiliza kesi hiyo amesema kuwa Detective Sergeant Nengea hawezi kuulizwa sawli lolote kwa kuwa yeye alikuwa anasoma ushahidi wa mtu ambaye uliandikwa na sio yeye ndio alikuwa shahidi.

Jaji huyo pia ameongeza kwa kusema kuwa kesho siku ya Alhamisi wazee wa baraza watakaa na kujadili kama Lulu ana hatia katika kesi hiyo inayomkabili au hana.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents