Michezo

Kilimanjaro Stars Yashindwa Kutakata Dhidi Ya Burundi

Kiungo hatari wa Kilimanjaro Stars Simon Msuva akijaribu kumfunga kipa wa Burundi.

Timu ya Soka ya Tanzania Bara inayoiwakilisha nchi katika michuano ya Tusker Challenge Cup, jijini Kampala, Uganda, Kilimanjaro Stars, jana jioni, imeshindwa kutamba mbele ya timu ya taifa ya Burundi, baada ya kukubali kipigo cha bao moja kwa bila katika mcheza wa pili wa kundi B.
BAO pekee lililowanyima furaha mashabiki, wapenzi na wadau wa soka nchini, ambao wengi wanafuatilia michuano hiyo kupitia luninga lilifungwa na mshambuliaji wa zamani wa Simba SC, Suleiman Ndikumana, katika dakika ya 52 ya mchezo huo.

Bao hilo lililopatikana kwa njia ya mkwaju wa penati, liliwekwa kimiani na nahodha wa timu ya taifa ya Burundi anayechezea katika timu ya nyumbani kwao Inter Stars. Mchezaji huyo alifunga bao hilo kwa njia ya penalti, baada ya yeye mwenyewe kuangushwa kwenye eneo la hatari na mchezaji wa Kilimanjaro Stars Shomary Kapombe.

Hadi kipindi cha kwanza kinakatika, hakuna timu iliyofanikiwa kuona lango la mwenzake na Burundi walifanya mashambulizi mawili ya hatari zaidi, lakini sifa zimuendee ‘TZ One’, Juma Kaseja aliyeokoa hatari hizo, pamoja na michomo mbali mbali.
Kilimanjaro Stars hawakucheza vizuri sana kutokana na hali mbaya ya Uwanja, kujaa matope, na kuwa wenye kuteleza kutokana na mvua kubwa iliyonyesha kutwa nzima ya jana. Kipindi cha pili Stars walijitahidi kutaka kusawazisha mabao hilo, lakini bahati haikuwa yao na zaidi waliishia kukosa mabao mawili ya wazi.
Kwa matokeo hayo, Burundi imeendelea kuongoza Kundi A, kwa pointi zao sita, mabao sita ya kufunga na moja la kufungwa, wakati Bara inabaki nafasi ya pili kwa pointi zake tatu, Sudan ya tatu ikiwa na pointi tatu na Somalia yenye pointi moja inashika mkia.
Kikosi cha Tanzania Bara leo kilikuwa; Juma Kaseja, Erasto Nyoni, Amir Maftah, Shomary Kapombe/Issa Rashid, Kevin Yondan, Frank Domayo, Mrisho Ngassa, Salum Abubakar, John Bocco, Mwinyi Kazimoto/Shaaban Nditi na Simon Msuva/Amri Kiemba.
Burundi; Arthur Arakaza, Gilbert Kaze, Haruna Manirakiza, Hassan Hakizimana, Emery Nimubona, Yussuf Ndikumana, Steve Nzigamasabo, Chris Nduwarugira, Suleiman NdikumanaChris Ndayishimiye na Amisi Tambwe.
Picha kwa hisani ya bongosta.blogspot.com

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents