Burudani ya Michezo Live

Kim Kardashian anataka Kanye West apate msaada wa kitaalam

Kim Kardashian anamtaka mume wake Kanye West apate msaada wa kitaalam, kwa mujibu wa ripoti ya US Weekly.

kanye-west-kim-kardashian-inline-9713cb7d-dc35-4b25-88ed-b44adef43271

Kim amefedheheshwa na tabia ya hivi karibuni ya mume wake ikiwemo diss yake ya Taylor Swift kwenye album ya The Life Of Pablo na kumuomba msaada wa kifedha, mwanzilishi wa Facebook, Mark Zuckerberg.

Chanzo kilicho karibu na familia yao kimedai kuwa Kim ana wasiwasi na tabia yake mume wake na wamekuwa na matatizo makubwa yanayokua kila siku.

Pamoja na Kim kumtaka mumewe ajirekebishe, rapper huyo bado ameendelea kuitumia Twitter kutoa malalamiko yake. Mapema mwezi huu iliripotiwa kuwa Kim amekuwa akichukizwa na kile mumewe anachopost kwenye Twitter.

Jumatano hii pia Kanye alilianzisha kwa kuwashambulia waandaji wa tuzo za Grammy.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW