Burudani

Rais wa Misri ‘auzwa’ kwenye mtandaoni wa ‘Ebay’ kwa dolla $100,000

Raia wa Misri wamekuwa wakimkejeli rais wao Abdul Fattah al-Sisi mtandaoni baada yake kusema kwamba anaweza kujiuza ili kusaidia uchumi wa taifa hilo.
160224213246_sisi_ebay_624x351_bbc_nocredit

“Ingeliwezekana mimi niuzwe, ningejiuza,” alisema Bw Sisi alipokuwa akihutubu kupitia runinga ya taifa.

Muda mfupi baadaye, ukurasa uliundwa kwenye mtandao wa kuuza bidhaa mtandaoni wa Ebay wa “kumuuza” Bw Sisi.

Kwenye ukurasa huo, uliofunguliwa dakika chache baadaye, muuzaji alisema akiuza “jemedari ambaye amemaliza muda wake wa kutumia” na kuweka picha ya rais huyo hapo.

Bei ilizidi $100,000 (£72,000) baada ya saa kadha. Ukurasa huo baadaye ulifutwa.

Bw Sisi alikuwa pia amependekeza Wamisri watoe “pauni 10 ($1.2; £0.9) kwa Misri kupitia ujumbe wa simu” kusaidia kupunguza mzigo wa kiuchumi unaokumba taifa hilo.

Alisema hayo alipokuwa akizindua mpango wa ukuaji wa kiuchumi wa 2030.

Matatizo yanayokabili Misri kwa sasa ni pamoja na kupungua kwa uwezekaji kutoka nje pamoja na kupungua kwa watalii.

Kiwango cha mfumuko wa bei nchini humo kimepanda sawa na ukosefu wa ajira.

Hivi vimetokana na miaka kadha ya machafuko.

Bw Sisi ameapa kuendelea kujenga nchi hiyo “hadi mwisho wa maisha yangu au muhula wangu” na kuwahimiza Wamisri wamsikize yeye pekee iwapo wanaipenda Misri kwa dhati.

“Msiwasikize wengine, nisikizeni mimi,” amewahimiza

Source:BBC

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents