Habari

Kitabu cha Kiswahili chenye mbinu 60 za kuupata utajiri chazinduliwa Dar

Imeelezwa kwamba watu wengi wamekuwa wakishindwa kufanikiwa kimaisha kutokana na kutokuwa na mipango ya kimaisha ambayo wanaweza kuifanyia kazi ili waweze kufanikiwa kama jinsi ilivyo kwa baadhi ya watu ambao wanaonekana kuwa na mafanikio.

14606922_318991251804373_8345719822381744128_n
Mwandishi wa kitabu cha TIMIZA MALENGO YAKO, Joel Nanauka (Kulia) akiwa na mmoja wa watu waliohudhuria kwenye uzinduzi

Hayo yamesemwa na Mwandishi wa kitabu cha TIMIZA MALENGO YAKO, Joel Nanauka wakati wa uzinduzi wa kitabu hcho ambacho kinnaelezea mbinu 60 ambazo zinatumiwa na watu waliofanikiwa kimaisha kuweza kufikia alengo ambayo wamejiwekeakatika maisha yao.

Nanauka alisema watu wengi wamekuwa wakitamani kufanikiwa lakini wamekuwa hawajui ni hatua gani za kupitia na kufanikiwa na baada ya yeye kufanya utafiti wa muda mrefu kwa watu mbalimbali duniani waliofanikiwa na wasiofanikiwa, ameweza kupata mbinu 60 ambazo ndiyo zinatofautisha watu wa matabaka hayo mawili

14693664_334937313538655_4520035844442030080_n
Nanauka akiwa na washereheshaji maarufu, MC Pilipili na MC Luvanda

Alisema kupitia kitabu hicho msmaji ataweza kufahamu ni mambo gani anatakiwa kufanya na yapi hatakiwi kufanya ili kufanikiwa kama wengine kwa kuzingatia mbinu ambazo pia zimekuwa zikitumiwa na watu waliofanikiwa katika nyanja mbalimbali kama biashara, michezo, sanaa na hata uongozi.

“Watu wengi wanapenda kufanikiwa lakini kama huna malengo huwezi kufanikiwa, watu wengi hawajui wanatumia njia gani ili kufanikiwa na hadi wanaondoka duniani wanaondoka na ndoto walizokuwa nazo, ndoto ambazo zilitakiwa kubaki zikifanya kazi duniani,

“Sababu ya kuandika kitabu hiki ilianza nipotaka kujua utofauti wa waliofanikiwa na wasiofanikiwa, aliyefanikiwa kwa aliye Marekani na Tanzania na asiefanikiwa aliye Tanzania a Mareani, nilianza kusoa kwanini wengine wanaweza kufanikiwa katikati ya mamilioni ya watu na baada ya kupata mawazo ya jumla ndiyo nikapata mbinu 60 ambazo zipo katika kitabu cha TIMIZA AHADI YAKO,” alisema Nanauka.

Nanauka alisema kitabu hicho kitakuwa kikuzwa kwa Tsh. 10,000 na anaamini kila ambaye ataweza kusoma kitabu hicho ataweza kupata kitu kipya ambacho kitaweza kumsadiakufanikiwa na kufika ndoto abazo anatamani kuzifikia.

“Matumaini yangu kila atakaesoma kitabu hiki maisha yake yabadilike kutokana na mambo ambayo atayasoma na kila mtu hatajutia kusoma kitabu hiki, nimekiandaa kwa muda mrefu kwa kufanya tafiti nyingi na kuweka mifano ambayo naamini itabadili maisha ya watu wengi wataokisoma,” alisema Nanauka.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents