Habari

Kituo cha uwekezaji chakanusha taarifa za gazeti la The Economist kuwa tangu Rais Magufuli aingie madarakani wawekezaji wa nje wanaikimbia TZ

Gazeti la Uingereza, The Economist, May 28 liliandika makala isemayo; Government by gesture: A president who looks good but governs impulsively.

20160528_mad001

Kwenye makala hiyo, gazeti hilo liliandika mambo mengi yanayohusu uongozi wa Rais Dkt John Pombe Magufuli ikiwemo namna alivyozuia safari za nje za maofisa, kupambana na wafanyakazi hewa, kuanzishwa kwa sheria na kodi kali kwenye bandari ya Dar es Salaam ambapo gazeti hilo limedai kuwakatisha tamaa wafanyabiashara wengi walioanza kutumia bandari za Kenya, Msumbiji na Afrika Kusini.

Likimnukuu bosi wa kampuni moja kubwa Afrika, gazeti hilo aliyedai kuwa Tanzania sasa imekuwa nchi isiyowekezeka tena.

Kutokana na habari hiyo, kituo cha uwekezaji Tanzania, TIC kimetoa ufafanuzi kuhusu hali ya uwekezaji nchini na kukanusha kile kilichoandikwa na gazeti hilo.

Katika taarifa yake kwa waandishi wa habari, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TIC, amedai kuwa tangu Rais Dkt Magufuli aingie madarakani December 5, 2015 hadi May 2016, TIC imesajili miradi 551 yenye thamani ya dola za Kimarekani milioni 9,211.88. Katika miradi hiyo, 229 inamilikiwa na Watanzania, 215 ikimilikiwa na raia wa kigeni, huku 107 ikimilikiwa kwa ubia. Taarifa hiyo imedai kuwa miradi hiyo inatarajiwa kuajiri watu 55,970.

Imesema uwekezaji huo umeonesha ongezeko la asimilia 20.31% ukilinganisha na miezi sita kabla ya Rais Magufuli haijaingia madarakani yaani June – November 2015 ambapo TIC ilisajili miradi 458 yenye thamani ya dola milioni 5,727.29 katika kipindi hicho.

TIC imesema uwekezaji nchini umeongezeka katika kipindi hiki cha utawala wa Rais Magufuli na kwamba wawekezaji wana imani na Tanzaia. Imetaja sababu kubwa la ongezeko hilo, ni nchi kuwa na sheria za kuvutia, amani, uthabiti, sera nzuri na rafiki pamoja na mazingira mazuri ya uwekezaji.

Pia taarifa hiyo imezungumzia kuhusu ripoti ya benki kuu ya dunia ya mwaka 2015 kuwa uwekezaji wa kigeni (FDI) kwa Tanzania uliongezeka kwa asilimia 14.5%.

“Hivyo kauli kuwa nchi yetu imekuwa isiyowekezeka kabisa haina ukweli na inatakiwa kupuuzwa vikali na umma na wasomaji,” imesisitiza taarifa ya TIC.

Bofya hapa kuisoma taarifa nzima ya TIC.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents