Michezo

Kiwango cha Donald Ngoma chamkuna Kocha wa Yanga

Kocha Mkuu wa Klabu ya Yanga, George Lwandamina ameonekana kukunwa na kiwango cha mshambulizi Donaldo Ngoma na kumuongeza kwenye orodha ya idadi ya washambuliaji anaowataka msimu ujao kitu kilichowaacha mashabiki midomo wazi.
Tokeo la picha la donald ngoma  Lwandamina
Donald Ngoma
Kauli hiyo ya Kocha imeanza kuwachanganya baadhi ya wadau na Mashabiki wa Yanga ambao awali walipata taarifa  kuwa Ngoma hata salia  Klabuni hapo mwishoni mwa msimu huu.
Mkataba wa Ngoma na Klabu ya Yanga umebakiza mwezi mmoja tu kuisha na uongozi wa Yanga ulitangaza kwamba mchezaji anayetaka kuondoka ruksa na kumekuwa na taarifa kuwa Ngoma yuko kwenye rada za watani wao wa Jadi Simba SC.
Habari za ndani kutoka Jagwani zinaeleza kuwa Lwandamina anataka washambuliaji wenye usumbufu kama wa Ngoma kwa kuwa anakuwa anawachosha mabeki wa timu pinzani .
By Godfrey Mgallah

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents