Michezo

Klabu ya soka ya wasichana yashinda ligi ya wavulana hispania

Klabu ya soka ya AEM Lleida ya nchini Hispania imewashangaza wengi baada ya kutwaa Ubingwa katika ligi ya wavulana. Maajabu haya yanatokea wakati watu wengi wakionekana kutokuunga mkono soka la wanawake nchini Hispania, hali iliyopelekea timu hiyo kushiriki ligi ya wanaume.

Wachezaji wa Klabu ya soka ya wanawake ya AEM Lleida wakishangilia Ubingwa

AEM Lleida, ilimwagiwa sifa na gazeti la The New York Times, wakati waandishi wa gazeti hilo walipokwenda kutembelea klabu hiyo iliposhinda kombe hilo katika ligi hiyo inayohusisha wachezaji chipukizi eneo la Lleida.

Klabu hiyo imejishindia michezo 21 kati ya 22 uwanjani. Nchini Hispania, timu za wasichana na wavulana haziruhusishwa kucheza pamoja hadi wachezaji wanapotimiza umri wa miaka 14.


Klabu ya ya soka ya wanawake ya AEM Lleida wakicheza na wavulana

Timu hiyo ya AEM Lleida imecheza dhidi ya klabu za wavulana tangu 2014, hata hivyo, hakukuwa na wadhamini wowote kwa timu yoyote ya soka ya wasichana.
Real Madrid, klabu tajiri zaidi Uhispania, haina timu ya wanawake.


Klabu ya ya soka ya wanawake ya AEM Lleida wakicheza na wavulana

“Ili kuwapa wasichana hawa msukumo, tulihisi kwamba walihitaji kucheza dhidi ya wavulana kwa sababu panahitajika upinzani hatari ndipo uweze kupiga hatua na kujiboresha,” Alisema Jose Maria Salmeron, mkurugenzi wa AEM Lleida alipoliambia New York Times

BY HAMZA FUMO

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents