Michezo

Kocha wa Taifa Stars afunguka baada ya kipigo cha goli tatu dhidi ya Cape Varde (Video)

Tanzania imeshacheza mechi 3 katika Kundi L imetoka sare mara 2 na kupoteza mchezo 1. Imefungwa magoli manne (4) na kufunga goli moja tu.

https://www.instagram.com/p/Bo2DagbBt76/?taken-by=tanfootball

Imebakiza mechi nyingine tatu ambapo itarudiana na timu zote tatu, Cape Verde na Uganda zitakuja uwanja wa taifa Dar huku Stars ikisafiri kwenda Lesotho kucheza na timu ya taifa hilo.

Taifa Stars imekukubali kipigo cha mabao 3-0 kutoka kwa Cape Verde katika mchezo uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa Capo, Mjini Praia.

Mabao ya Cape Verde mawili yaliyofungwa na mshambuliaji Ricardo Gomes kabla ya Yanique Tavares kuhitimisha kwa bao tatu.

Mshambuliaji wao, Ricardo Gomes anayekipiga nchini Serbia katika klabu ya Rartizan ndiye alipachika mabao hayo katika dakika ya 16 na 23 akitumia vizuri uzembe wa mabeki wa Stars, David Mwantika na Hassan Kessy, kabla ya Tavares kumalizia la tatu dakika ya 84 kwa shambulizi la kushtukiza.

Kocha wa timu ya Taifa Emanuel Amunike hiyo hiyo imepokeza mchezo huo baada ya kucheza vibaya katika kipindi cha kwanza baada ya kuruhusu wagoli mawili ya haraka.

“Tulipoteza mechi kipindi cha kwanza, lakini bado tuna nafasi tunaenda kujipanga zaidi kwaajili ya mchezo wetu wa nyumbani” -Kocha wa Taifa Stars, Emanuel Amunike.

Washambuliaji Stars wakiongozwa na nahodha Mbwana Samatta walishindwa kabisa kutumia nafasi chache walizopata kupata mabao.

Kutokana na matokeo hayo, Cape Verde inapanda mpaka nafasi ya kwanza ya Kundi L iliyokuwa inakaliwa na Uganda ‘The Cranes’ kwa kuwa na idadi kubwa ya mabao, Lesotho ya tatu na Taifa Stars inashika mkia.

Cape Verde na Uganda wana idadi ya pointi sawa ambazo ni nne. Uganda watacheza mchezo wao wa tatu kesho Jumamosi na Lesotho.

Taifa Stars inatarajiwa kucheza mchezo wa marudiano na Cape Verde Jumanne ijayo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents