Habari

Kocha wa timu ya taifa, taifa stars aagwa rasmi

Aliyekuwa kocha Mkuu wa Taifa Stars, Marcio Maximo, ameagwa rasmi usiku wa kuamkia leo katika hafla fupi iliyoandaliwa na TFF Msasani jirani na shule ya Feza jijini Dar . Katika hafla hiyo, pamoja na mambo mengine, Kocha Maximo alipewa zawadi mbalimbali ikiwemo ya kinyago alichopewa na Mwenyekiti Mtendaji wa kiwanda cha Serengeti, Jaji Mark Bomani.

Ni dhahiri kwamba kocha huyo atakumbukwa kwa kazi yake aliyoifanyia Tanzania japokuwa bado kuna wadau wa soka ambao wanasema hakufaya kitu ila tunaojua kusema asante tunasema Maximo amefanya kitu kikubwa katika soka letu lililokuwa la kichwa cha Mwendawazimu enzi hizo, na anastahili kupongezwa mpaka hapa alipotufikisha manake kuna methali inayosema “Mnyonge Mnyongeni lakini haki yake mpeni”

 

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents