Habari

Kuboresha Malipo ya Ada za Shule: Benki ya Exim Yazindua huduma ya ‘Exim Smart Shule’

Katika juhudi za kuboresha teknolojia za kidijitali katika sekta ya elimu, Benki ya Exim imezindua huduma ya ‘Exim Smart Shule’ maarufu kama’Shule Kidijitali’, suluhisho la malipo linalorahisisha malipo ya ada za shule moja kwa moja na wazazi, walezi, au wanafunzi wenyewe. Kupitia namba maalum inayotolewa na mfumo, malipo yanaweza kufanyika kwa urahisi kupitia matawi ya Exim Bank, Exim Wakala, na mitandao ya simu za mkononi. Mpango huu unalenga kurahisisha michakato ya malipo ya ada, kukuza ufanisi na upatikanaji wa huduma zamalipo ya ada za shule.

Eugen Massawe (kati), Mkuu wa Uendeshaji wa Matawi katika Benki ya Exim akielezea kuhusu huduma mpya ya benki hiyo ijulikanayo kama Exim Smart Shule, Shule Kidijitali itakayowezesha mzazi au mlezi kumlipia mwanafunzi ada ya shule kidijitali kupitia matawi ya benki hiyo, Exim Wakala na simu za mikononi. Kushoto ni Ramadhan Mbaga pamoja nae ni Elizabeth Mayengoh wote kutoka Exim Bank wakiwa katika uzinduzi wa huduma hiyo uliofanyika tarehe 20 Mei 2024 katika Makao Makuu ya benki hiyo jijini Dar es Salaam

“Huduma ya ‘Exim Smart Shule’, inaonesha adhima yetu yakuwa wabunifu kwa kukuza ujumuishaji wa kifedha wa kidijitali na kuendelea kuungana na wateja wetu. Mzazi au mlezi ataomba tu namba maalum ya udhibiti kutoka shuleni ili aweze kufanya malipo kwa urahisi na usalama,” anasema Eugen Massawe, Mkuu wa Operesheni wa Matawi wa Exim Bank.

Exim Smart Shule ina faida kadhaa kwa taasisi za elimu, wanafunzi, wazazi na walezi kwa kuunganisha teknolojia na huduma za kifedha katika sekta ya elimu. Jukwaa hili linarahisisha mchakato wa malipo ya ada, kufanya iwe haraka na yenye ufanisi zaidi kwa wazazi na uongozi wa shule.

Ramadhan Mbaga, Mkuu wa Kitengo cha Bidhaa za Kidijitaliwa Exim Bank, anasema, “Kupitia Exim Smart Shule, wazazi na wanafunzi wanaweza kufanya malipo kwa urahisi kwa kutumia njia mbalimbali kama vile matawi yetu ya Benki ya Exim, Exim Wakala, na mitandao ya simu.”

Kutumia huduma hili pia kunaleta ufanisi kwa sababu kila namba ni ya kipekee kwa kila mwanafunzi kwendana namuamala wa malipo. Hii husaidia kuhakikisha kuwa malipo yanawekwa kwa usahihi katika akaunti ya mwanafunzi husika, kupunguza uwezekano wa kukosea namna ya kufanyamalipo bila kuchanganya hesabu.

Matumizi ya Exim Smart Shule yanaweka uwazi katika mchakato wa malipo ya ada. Wazazi hupokea taarifa yamiamala ya malipo yao na kuthibitisha kuwa yamekamilishwa kwa mafanikio.

‘Exim Smart Shule’ inarahisisha malipo ya ada kwa wazazi, walezi, au wanafunzi kwa njia mbalimbali ikiwemo mtandaomkubwa wa matawi ya  benki hiyo, mitandao ya simu za mkononi, na vituo vyake vya mawakala maarufu kama ‘Exim Wakala’ vilivyosambaa kote nchini. Urahisi huu unamuwezesha mhusika kufanya malipo kwa urahisi akiwapopote bila kuhitaji kufika kwenye shule.

Kifedha, mfumo huu ni salama na wa uhakika katika kufanyamalipo ya ada kwa kutoa utambulisho maalum kwa kila muamala uliofanywa. Hii husaidia kupunguza uwezekano wamtu kuingia kwenye akaunti ya mzazi bila idhini nauwezekano wa wizi.

Kupitia Smart Shule, wazazi na walezi watakuwa na uwezo wa kupata ripoti kuhusu watoto wao, kalenda ya mwaka ya shule, na mfumo wa kufuatilia usafiri wa wanafunzi. Aidha, wanafunzi watafaidika na maktaba iliyojaa vitabu vya kusomaili kuwasaidia kufanya vizuri katika masomo yao.

“Kupitia huduma hili, Benki ya Exim inasaidia shule zilizojiunga na mfumo huu kutumia namba maalum kwa kilashule kwa ajili ya kufanya malipo. Hii inapunguza mzigo kwa utawala wa shule na kuhakikisha rekodi za shule ziko sawa,” anasema Elizabeth Mayengoh, Meneja wa Kanda kutokaExim Bank.

‘Exim Smart Shule’ ni hatua muhimu katika kuelekea katikaufanyaji wa malipo ya ada za shule kidijitali, ikitoa urahisi, ufanisi, na usalama kwa wazazi, walezi, wanafunzi, na taasisi za elimu. Huduma hili bunifu inaonesha namna ambavyoExim Bank inaamini katika ujumuishwaji wa kifedha kidijitalina mchango wake katika sekta ya elimu nchini. Ni Ushahidi mwingine wa kaulimbiu ya Exim Bank kuwa ‘Ubunifu nimaisha’.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents