BurudaniHabari

Kufanikiwa kwa MfALmE 2006

 Darda King Msanii Darda King (Mfalme) mwenye kufanyia kazi zake za muziki nchini marekani,ametua nchini kwa ajili ya utambulisho wa albam yake ya pili iitwayo (Nimekubalika 2006).

Msanii Darda King (Mfalme) mwenye kufanyia kazi zake za muziki nchini marekani,ametua nchini kwa ajili ya utambulisho wa albam yake ya pili iitwayo (Nimekubalika 2006).

Akiongea kwa furaha alipotinga ndani ya ofisi za DHW,msanii huyo alisema albam yake hii ya pili ina songi 12 na yote ikiwa ni kazi kutoka ndani ya studio yake mwenyewe ya Mfalme Records.

Darda King na wachumba.

Akiielezea albam hiyo msanii huyo anasema ni moja kati ya albam nzuri zilizowahi kufanywa na msanii mtanzania aishiye nje ya nchi na kuzitaja track ambazo ziko hewani sasa hivi kuwa ni YIHO na DAR.

Kwa mujibu wa Darda…albam hii ilianza kuuzwa marekani tangu February mwaka huu na hivi sasa anafanya mazungumzo na kampuni moja ya jijini ili iweze kuwa mwakilishi ktk kusambaza kazi zake kwa hapa nchini.

Msanii huyu ambaye jina lake halisi ni Dardanus Mfalme alisema kabla hajarudi unyamwezini anatarajia kuandaa party ndogo kwa ajili ya kuitambulisha albam hiyo kwa wadau wa muziki na pia ataendesha semina ndogo ya kuwaelimisha wasanii wa Bongo namna ya kuufanya muziki wao uweze kuuzwa kwenye soko la kimataifa.

Alizitaja songi zilizomo kwenye albam yake kuwa ni…Jijini Dar,Kunazi,Tulingeba,Zaburi 23,Kaburu (Interlude),Yiho,Elimu Africa na Mjane.

Zingine ni Simu,Ulivyotaka,Umeniacha, pamoja na Nimekubali.

Kazi za msanii huyu pia zinauzwa ktk website kubwa hapa duniani kama vile…Amazon.com,CdBaby.com,CDnow.com na Borders.com.

Darda alimalizia kwa kusema kuwa muziki wake umepata nafasi ya kuuzwa kwenye website hizo kutokana na kufanyiwa Mastering ya uhakika na wataalam wa hali ya juu kutoka studio za Music House Mastering za New York ambapo kazi yote hiyo ilisimamiwa na mkali aliyemtaja kwa jina la Michael Dominici.

 

 

SOURCE: Darhotwire

{mos_sb_discuss:6}

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents