Kumbe Richmond ni ya Ukweli!?

Kampuni ya Richmond Development ambayo ilipewa dhamana ya kuagiza mitambo ya kuzalisha umeme wa dharura na shirika la umeme Tanesco hivi karibuni imesema hawahusiki na haikuwahi kupokea fedha yoyote kutoka serikalini

Kampuni ya Richmond Development ambayo ilipewa dhamana ya kuagiza mitambo ya kuzalisha umeme wa dharura na shirika la umeme Tanesco hivi karibuni imesema hawahusiki na haikuwahi kupokea fedha yoyote kutoka serikalini na kwamba kampuni yao ni halali na imesajiliwa kihalali nchini Marekani.


 


Akizungumza na waandishi wa habari mwanasheria wa kampuni hiyo Bw. Cuthbert Tenga amesema, yote yaliyotolewa na kamati ya bunge juu ya kutokuwepo kwa kampuni hiyo si ya kweli kwani imesajiliwa kwa faili namba 1019936 mnamo tarehe 10 mwezi wa sita mwaka 2004 mjini Huston Marekani.


 


Amesema kimsingi kampuni ya Richmond ilishindwa kuendelea na mkataba wake dhidi ya Tanesco na kuiachia kampuni ya Dowans kwa kile kilichodaiwa kushindwa kufanya kazi katika mazingira ya maeneo yasiyo na msingi.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents