Habari

Kushambuliwa kwa vituo vya mafuta Saudi Arabia kwapandisha bei ya nishati hiyo, Marekani yaidai Iran yahusika na tukio hilo

Gharama ya mafuta imepanda kwa kiwango cha juu kuwahi kushuhudiwa katika miezi minne baada ya mashambulio mawili dhidi ya vituo vya mafuta Saudi Arabia Jumamosi yaliosababisha kumwagika kwa 5% ya mafuta duniani.

Smoke is seen following a fire at Aramco facility in the eastern city of Abqaiq

Kiwango cha mafuta ghafi yalipanda kwa 19% kwa thamani ya $71.95 kila mtungi huku viwango vingine, West Texas Intermediate, vikipanda 15% kwa thamani ya $63.34.

Bei zilishuka kidogo baada ya rais wa Marekani Donald Trump kuagiza kufunguliwa kwa akiba nchini Marekani.

Huenda ikachukua wiki kadhaa kabla ya vituo hivyo Saudia kurudi katika hali ya kawaida.

Mashambulio hayo dhidi ya vinu katika shina la viwanda vya mafuta Saudia vinajumuisha kituo kikubwa duniani cha usafishaji mafuta.Fire at Saudi oil facility

Moto uliozuka katika kituo cha mafuta Saudia mwishoni mwa juma

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Mike Pompeo amesema Tehran imehusika na mashambulio hayo. Iran imeishutumu Marekani kwa ‘uongo’.

Baadaye Trump amesema katika ujumbe wa Twitter kuwa Marekani inafahamu mhusika wa uhalifu huo ni nani na ipo tayari ila inasubiri kusikia kauli ya wa Saudi kuhusu namna ambavyo inataka kulifuatilia hili.Ujumbe wa Twitter wa @realDonaldTrump: Saudi Arabia oil supply was attacked. There is reason to believe that we know the culprit, are locked and loaded depending on verification, but are waiting to hear from the Kingdom as to who they believe was the cause of this attack, and under what terms we would proceed! 

Katika ujumbe mwingine kwenye twitter, amesema ” kuna mafuta mengi!”.

Athari yake kwa usambazaji mafuta ni ipi?

Wasaudi hawajaeleza kwa kina kuhusu mashambulio hayo, kando na kusema kwamba hakuna aliyeathirika, lakini imetoa ishara kidogo kuhusu utengenezaji mafuta.

Waziri wa nishati mwanamfalme Abdulaziz bin Salman amesema kupungua kwa utengenezaji mafuta kutafidiwa kwa kutumia akiba kubwa iliopo.

Ufalme huo ndio wauzaji wakuu wa mafuta duniani, ambapo unasafirisha zaidi ya mitungo milioni 7 kwa siku ya mafuta.

“Maafisa wa Saudia wamedai kudhibiti moto huo, lakini sio kuwa umezimwa kikamilifu,” amesema Abhishek Kumar, mkuu wa takwimu katika shirika la Interfax Energy mjini London. “Uharibifu kwa vituo vya Abqaiq na Khurais unaonekana kuwa mkubwa, na huenda ikachukua wiki kadhaa kabla ya usambazaji mafuta ukarudi katika hali ya kawaida.”

Saudi Arabia inatarajiwa kutumia akiba ili usafirishaji mafuta uendelee kama kawaida wiki hii.

Hatahivyo, Michael Tran, mkurugenzi msimamizi wa mipango ya nishati katika soko la RBC Capital Markets mjini New York, amesema: “hata iwapo tatizo hilo litatatukiwa kwa haraka, tishio la kutenga 6% ya mafuta yanayotengenezwa duniani sio fikra tu. Kutahitajika, faida ya ziada inayohitajika kwa mwekezaji kujilipa.”Saudi Arabia with capital Riyadh, the two oil facilities Abqaiq and Khurais, Yemen to the south and Iraq and Iran to the north

Mashambulio yalilenga vituo vya Abqaiq na Khurais Saudi Arabia ya kati

Marekani inatuhumu nini?

Bwana Pompeo amesema Tehran imehusika na mashambulio hayo ya uharibifu lakini hakutoa ushahidi maalum kuunga mkono tuhuma zake.

Amepinga tuhuma za waasi wa Houthi nchini Yemen wanaoungwa mkono na Iran kwamba wao ndio waliotekeleza mashambulio hayo.

Iran imeishutumua Marekani kwa ‘uongo’ na waziri wake wa mambo ya nje Javad Zarif amesema kuwa “kuituhumu Iran hakutomaliza janga” nchini Yemen.

Yemen imekumbwana vita tangu 2015 wakati rais Abdrabbuh Mansour Hadi alipolazimishwa na waasi hao wa Houthi kutoroka mji mkuu Sanaa. Saudi Arabia inamuungamkono rais Hadi, na imongoza muungano wa mataifa ya kieneo dhidi ya waasi hao.

Wakati huo huo Marekani imeituhumu Iran kwa mashambulio mengine katika vituo vya mafuta katika enoe hilo mwaka huu, huku kukishuhudiwa wasiwasi kufutaia uamuzi wa Trump kuidhinisha upya vikwazo baada ya kujitoa katika makubaliano muhimu ya kimataifa yaliodhibiti shughuli za nyuklia za Tehran.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents