Michezo

Kwa nini hawaniachi niende ? – Diego Costa

Mshambuliaji wa klabu ya Chelsea ya nchini Uingereza, Diego Costa amesema kuwa meneja, Antonio Conte alikuwa akimchukulia kama mualifu ndani ya kikosi hicho.

Diego Costa akiwa amemualika muandishi wa michezo nyumbani kwake kwaajili ya Mahojiano siku ya Jumamosi

Costa mwenye umri wa miaka 28, ambaye ameichezea Chelsea katika kaifanali ya michuano ya FA Cup mwezi May, alitumiwa ujumbe kutoka kwa Conte uliyomtaka kuachana na kikosi hicho mara baada ya kuanza kwa msimu mpya.

Costa akiwa anaiangalia timu yake ya Chelsea ikifungwa na Burnley katika mchezo wa ufunguzi wa  the Premier League

Mshambuliaji huyo ameliambia gazeti la Daily Mail kuwa “Kwanini hawaniachi niondoke kama hawanihitaji. Ninafanya ninachopaswa kufanya, nahitaji kukaa na kufikiria hili. Nimekuwa kijana mzuri hapa na kufanya yaliyomazuri na sasa matamanio yangu nikwenda Atletico.” Amesema Costa.

Costa (kulia)  akizungumza na muandishi  Adam Crafton (kushoto) kuhusu maisha yake ya baadae katika mchezo wa soka

Costa amejiunga na Chelsea akitokea katika klabu ya Atletico Madrid ya Hispania mwaka 2014 na kushinda mataji mawili ya Ligi Kuu ya nchini Uingereza na la League Cup.

Mwezi Januari aliachana na Chelsea ilipokuwa katika mchezo dhidi ya Leicester baada ya kuhusishwa kuwepo na mgogoro na kocha wake, Antonio Conte.

Mshambuliaji huyo ameongeza kuwa “Mwezi Januari nilipohitaji kuongeza mkataba wangu ikashindikana naamini kocha ndiye aliyeweka kikwazo”.

“Mtazamo wake upo wazi na haubadiliki namuona yeye ni mtu wa namna gani sasa na mwenye mitazamo binafsi isiyobadilika.
“Ninamheshimu kama kocha mwenye uwezo mkubwa na ambaye amefanya kazinzuri ila binafsi yeye sio mwalimu ambaye yupo karibu na wachezaji wake”.

By Hamza Fumo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents