Bongo5 MakalaBurudani

Kwanini sio sahihi kwa Mswaki kuruhusiwa kuchukua ‘identity’ ya Ngwair kutumia kibiashara

Producer Mswaki anataka kuchukua uamuzi ambao tangu nianze kufuatilia muziki, sijawahi kuusikia. Ni uamuzi wa kuchukua ‘kisheria’ ‘character’ ya marehemu Albert Mangwair na kuitumia kibiashara.

14ba299eab4c11e39ffb0ad53a0c46c6_8
Mswaki (aliyenyoosha mkono) akiwa na wenzake waliosafiri kwenda Morogoro kuomba kibali cha kutumia mtindo wa rap ya Ngwair kwa mama yake Albert

Kama ataruhusiwa na mama yake mzazi Mangwair, Mswaki kupitia mradi wake alioupa jina ‘Keeping Ngwair Alive’ atakuwa akirap kwa kutumia mtindo na sauti ya Ngwair. Kufanikisha hilo, wiki hii producer huyo alisafiri hadi mjini Morogoro kumuona Mama mzazi wa Ngwair ili kumuomba kibali cha kufanya hivyo. “Thank you Lord tumerudi salama….Kuhusu alichokisema Mama Albert utakijua soon…. #KeepingNgweaAlive,” ameandika Mswaki kwenye Instagram.

d01b121caaec11e384fd0e57c4636331_8

Mimi ninavyo hisi hiki kitu kinaweza kuwa na faida gani kwa muziki wa Albert na yeye aone kama ataona sawa aseme kama ni sawa ninaweza nikaendelea kuifanya au kama sio sawa,“Mswaki aliiambia XXL ya Clouds FM kabla ya safari hiyo.

“So kama akisema ni sawa mimi nitajua naipush kwa ukubwa gani kunzia ila nataka kwanza nimsikie yeye mwenyewe binafsi. Familia ita benefit percent nitagawa percent sijajua mpaka sasa hivi ni percent ngapi? Iwe 50-50, mimi nitagenga some of my time nitapanga ratiba yangu vizuri tu ya kazi zangu zisiingiliane kwasasabu huko itabidi ni act kama msanii sasa unajua kuna ma interview, shows kuna nini ,na upande mwingine mimi ni music producer kwahiyo itabidi nipange ratiba yangu sawa niko radhi kuipanga ratiba yangu kihivyo ili tu hiki ninachokifanya kifike pale ambapo mimi naona ni sawa ni sehemu sahihi.”

Sifahamu Mswaki na Magwair walifahamiana lini ama huo ukaribu wao ulianzia wapi lakini inavyoonekana Ngwair ni mtu aliyemuinspire sana Mswaki. Kwangu mimi sasa naanza kuiona inspiration hiyo imeanza kuwa obsession kwa Mswaki.

Tayari Mswaki alishafanya wimbo uitwao Open Letter aliochana kwa style ya Ngwair kama tribute kwake na kwakuwa ni kweli kwa kiasi fulani anaweza kuipatia sauti ya marehemu, watu wengi waliupenda. Nahisi kukubalika kwa wimbo huo, kulimtamanisha zaidi Mswaki aliyeamua kuichukulia serious.

Sina nia ya kumkatisha tamaa Mswaki katika hili, lakini kuna vitu viwili tu vinavyoniingia akilini mwangu na kuitafsiri project hii; obsession na kutafuta kiki. Hata kama nia anayoielezea yeye ni kuendeleza ‘legacy’ ya Ngwair, sioni kama hii ni njia nzuri ya kufanya hivyo. Infact, badala ya kuendeleza urithi wa Ngwair, nahisi mradi wake unaweza ukafanya kinyume chake.

Bado nyimbo za zamani za Ngwair zitaendelea kutupa fursa hiyo ya kumuenzi. Bado kuna nyimbo mpya za ‘Ngwair halisi’ zinazotarajiwa kutoka na isitoshe hivi karibuni tu wimbo wake mpya ‘Alma’ uliachiwa. Bado kuna album mpya ya Ngwair itakayotoka kupitia Bongo Records na itakayokuwa na nyimbo nane. Hiyo ina maana kuwa kutakuwa na nyimbo nyingi mpya za ‘Ngwair Halisi’, kwanini mashabiki wake wasikilize nyimbo za ‘Ngwair Wannabe’?

Sina lengo la kubeza mradi wa Mswaki lakini nahofia inaweza kuwa na madhara kwenye miradi halisi ya Ngwair. Nahisi njia nzuri ya kumuenzi Ngwair ni kwa kusikiliza sauti yake halisi na sio sauti inayomuigiliza. Ngwair ni miongoni mwa wasanii wa hip hop wakali mno kuwahi kutokea Afrika, hakuna mtu anayeweza kuwa kama yeye, hakuna.. Ngwair atabaki kuwa Ngwair. Viatu vya Ngwair ni vikubwa mno kwa Mswaki, hawezi kuvivaa.

Njia bora aliyotakiwa kuifanya Mswaki ni kwa kutumia uwezo wake kama producer, kutengeneza ladha mpya ya nyimbo za Ngwair na kuziongezea utamu. Kuna uwezekano, akiongea vizuri na watayarishaji waliowahi kufanya kazi na Ngwair wakampa acapella zake na yeye kuzitengenezea muziki mwingine wa tofauti. Hiyo ndio njia sahihi ya kumuenzi Ngwair, that’s the best way of keeping Ngwair alive. Isitoshe, hivyo ndivyo wasanii kama Michael Jackson, Whitney Houston, Aaliyah ama Left Eye wanaenziwa.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents