Burudani

LA Reid ajiuzulu Epic Records

Antonio Marquis maarufu kama L.A. Reid amejiuzulu katika nafasi yake ya uwenyekiti wa lebo ya Epic Records.

L.A. Reid alianza kufanya kazi na lebo hiyo iliyopo chini ya Sony Music kuanzia Julai 2011, na katika kipindi hicho chote, amefanikiwa kuwasaini mastaa kama Future, Jennifer Lopez, Diddy, DJ Khaled, Travis Scott, Fifth Harmony na Meghan Trainor.

Pia bosi huyo alifanikiwa kumrudisha Mariah Carey katika himaya ya Sony Music kutoka Island Def Jam alipokuwa amekimbilia mwanzoni.

Dj Khaled ameonekana kuumizwa kwa kuondoka kwa Reid, kupitia mtandao wa Instagram, ameandika, “Bless up @la_reid bless up from me @wethebestmusic and the @epicrecords team !.” Hata hivyo bado haijafahamika sababu ya L.A. kuamua kuachia ngazi.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents