DStv Inogilee!

Lady Jaydee ajibu maswali ya mashabiki, akaribisha wanaotaka kazi

Kupitia blog yake Lady Jaydee amejibu maswali ya mashabiki waliomuuliza kupitia ukurasa wake wa Facebook. Hivi ndivyo alivyoandika:

Kama nilivyoahidi kujibu maswali ya walio andika facebook inbox. Ambayo mengi yao yana fanana, ila kwa yale ambayo yatakuwa hayajajibiwa ni kutokana na kuwa sikupata majibu yake. Au sina majibu yake kabisa.

1. WANAOOMBA KUFANYA NYIMBO ZA KUSHIRIKIANA, COLLABO/FEAT

Jibu: Ningependa kufanya nyimbo nyingi kwa kushirikiana na wasanii tofauti, lakini kutokana na ukweli halisi ni kwamba Duniani popote. Haiwezekani kwa msanii yoyote kufanya Collabo na kila msanii anaeomba kufanya nae.
Hii ni kutokana na kwamba hata wasikilizaji watachoka kusikia kila siku sauti ya mtu huyo huyo mmoja kwenye kila wimbo. Pia wakati mwingine inahitajika kuupa muda katikati ya Collabo na Collabo.

Na ni vema kuwa niwe nimeshawahi hata kumsikia mtu ambae anaomba nifanye nae wimbo.
Mengi mengine yanakuwa nje ya uwezo wangu.

2. WANAOTAKA KUWA MEMBER WA LA FAMILLE

Jibu: Vigezo vya kuwa member ni kwa wale ambao tumekuwa tukishirikiana nao kwa mambo mbali mbali katika mitandao, tukazoeana baadae tukakutana uso kwa uso na kujenga undungu.
Kwasasa tunaiboresha Familia iliopo, watu wazoeane na kufahamiana kwa ukaribu kabla ya kuongeza members wengine wapya.

Nilifikiria kuunda kundi la pili, litakaloitwa LA FAMILLE 2
Ili lile la kwanza libakie kuwa vile vile, kwakuwa wamekwisha zoeana sana
Na la pili waunde mazoea pia uwe ni umoja mwingine.

3. WANAOOMBA KUWA NDUGU ZANGU WA HIARI -DADA, KAKA, WADOGO

Jibu: Mtu yoyote ambae anapenda kuwa ndugu yangu kwa hiari yake anakaribishwa. Tatizo linakuja pale anapotaka tuwe tuna chat muda wote
Ku chat haitawezekana kutokana na muda kuwa hautoshi.
Ila kunipenda na kuniandikia ni vizuri, nikipata muda nitakuwa najibu, Mkitaka kunitembelea, karibuni Nyumbani Lounge….Sina maneno….Karibuni sana

4. NAFASI ZA KAZI

Jibu: Kuhusiana na wanaohitaji nafasi za kazi
Mnaweza kuandika e-mail: [email protected]
Huko mtapata majibu kutoka kwa wahusika.

5. MISAADA

Jibu: Kwa wale wanaoniomba misaada ya pesa, za ada, chakula na mahitaji mengine.
Ukweli ni kwamba uwezo wangu sio mkubwa sana wa kuweza kumsaidia kila mtu.
Japo ningependa kusaidia, na huwa nasaidia pale ninapoweza.
Bahati mbaya maombi yamekuwa mengi kuliko uwezo wangu.

Misaada ya kimuziki naweza kutoa ushauri, ila sina uwezo wa kumlipia Studio kila msanii mchanga anaeniomba.
Ila mnaweza kwenda kwa wenye Studio zao wakawasaidia kuwarekodi bure, endapo watavutiwa na kazi zenu ila hiyo itakuwa ni kazi kwenu kuwashawishi kuwa mna vipaji na mnastahili kusaidiwa bure bila malipo yoyote

6. VIDEO MPYA
Jibu: Itatoka baada ya wiki moja

8. PROJECT NYINGINE ZINAZOKUJA
Jibu: Kwa sasa kuna project iko njiani na itaanza kuonekana mnamo mwezi wa October katikati.Nitawafahamisha pindi kila kitu kitakapokuwa tayari.

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW