Moto Hauzimwi
Shinda na SIM Account

Lady Jaydee apata uongozi mpya baada ya kutemana na Seven Mosha

Malkia wa muziki wa Bongo Flava, Lady Jaydee amefanikiwa kupata uongozi mpya ambao utasimamia kazi zake za muziki baada ya kuachana na Seven Mosha.

Akiongea na Bongo5, mtu wa karibu wa msanii huyo amethibitisha hilo kuwa Jide kwa sasa amepata uongozi huo mpya wa kampuni kutoka Nigeria ambao wanafanya kazi nchini Kenya.

Chanzo hiko kimesema kampuni hiyo inafahamika kama Taurus Muzik ambayo pia inafanya kazi na wasanii kama Dela Maranga na Kagwe Mungai (wote kutoka Kenya), na Urban Hype kutoka Zambia.

Tayari inadaiwa kuwa Jaydee ameshaanza kufanya kazi na kampuni hiyo na watatoa taarifa rasmi hapo baadae. Jide atatarajiwa kuwa na ziara ya muziki nchini Afrika Kusini mwezi Disemba mwaka huu.

Leave a comment

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW