Burudani

Lamar awachana watayarishaji wa muziki nchini

Mtayarishaji wa muziki Lamar kutoka Fish Crab amewachana watayarishaji wa muziki wa sasa.

Lamar amekiambia kipindi cha Planet Bongo cha EA Radio, watayarishaji wa sasa kila mmoja anajiona ni mkubwa wanashindwa kupeana ushirikiano ndio maana hata midundo yao mingi inafanana.

“Producers wa sasa wana kitu wenyewe wanakiita ‘ego’ kiasi kwamba wanashindwa hata kupatiana ushirikiano ndiyo maana ukisikiliza wimbo huu unafanana na ule, hata ule mzuka ambao zamani ukisikiliza nyimbo unapata hakuna, lakini zamani ukisikia wimbo alofanya Majani, Dunga au Master Jay lazima kuna kitu cha tofauti utakipata,” amesema Lamar.

“Zamani Majani mpaka akukubali ufanye naye kazi inabidi uwe na adabu lakini pia uwe na kitu cha pekee cha kumshawishi ndiyo maana hata nilivyoondoka kwake niliweza kufanya kazi na Dunga na waandaji wengine wanne tofauti kitu ambacho kilinipa ujuzi mkubwa kabla ya kuanzisha lebo yangu mwenyewe,” ameongeza.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents