Burudani

Lebo ya Kaka Empire ya King Kaka yaungana na UNICEF kusaidia vijana Kenya

Kampuni inayosimamia wasanii ya nchini Kenya Kaka Empire inayomilikiwa na rapper King Kaka imefanikiwa kuungana na shirika la Unicef kwaajili ya kutoa elimu ya maambukizi ya Ukimwi kwa vijana.

unnamed

Zaidi ya watu 1.5 milioni wanadaiwa kuwa na maambukizi ya virusi vya ukimwi nchini humo na asilimia 20 kati ya wagonjwa hao ni vijana waliokuwa na umri wa miaka 15-24.

Akiongea baada ya kusaini mkataba huo, King Kaka amesema, “Nina furaha sana kuwa mjumbe wa Unicef nitakuwa tayari kuchukua ujumbe kwa watu wengi duniani kote. Sisi wote tumeathjirika na HIV, tunamjua mtu anayeishi na HIV, rafiki anajua mtu ambaye anajua mtu. Tunapaswa kuwa na uwezo wa kuzungumza kuhusu suala hilo na kuwatia moyo wengine kuzungumza kwa uwazi.”

Naye mwakilishi wa shirika hilo nchini Kenya, Werner Schultink amesema kuwa wanafurahi kushirikiana na wasanii wenye vipaji kutoka Kaka Empire pamoja na kushirikiana na UNAIDS kwa kushirikiana kutoa elimu kwa vijana watafanikiwa kuutokomeza kabisa ugonjwa huo nchini humo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents