Habari

Leo ni mwaka mmoja tangu Sharo Milionea afariki kwa ajali ya gari

Kifo cha aliyekuwa mchekeshaji na mwanamuziki wa Bongo Flava, Hussein Mkieti aka ‘Sharo Milionea’ kimetimiza mwaka mmoja leo. Sharo alifariki dunia tarehe kama ya leo, majira ya saa mbili usiku kufuatia ajali mbaya ya gari.
sharo-milionea

Alikuwa safarini akitokea Dar es Salaam kuelekea nyumbani kwao katika kijiji cha Lusanga, Muheza mkoani Tanga.

Msanii huyo alikuwa akiendesha gari aina ya Toyota Harrier lenye namba za usajili T478 BVR na kupata ajali katika eneo la Songa- Maguzoni wilaya ya Muheza mkoani Tanga.

Marehemu alikuwa peke yake kwenye gari ambapo mchoro wa ajali ulionesha kuwa gari lake liliacha njia kabla ya kupinduka mara kadhaa.

Mazishi yake yalifanyika siku mbili baadaye. RIP.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents