MichezoUncategorized

Liverpool yaanza kuchechemea UEFA yapata pigo la mchezaji tegemezi

Liverpool yaanza kuchechemea UEFA yapata pigo la mchezaji tegemezi

Kiungo wa kati wa Liverpool Naby Keita alikimbizwa hospitalini baada ya kuondolewa uwanjani kwa machela alipoumia akicheza mechi ya Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya dhidi ya Napoli hatua ya makundi. Keita, aliyejiunga na klabu hiyo kutoka RB Leipzig ya Ujerumani kwa £48m majira ya joto mwaka huu, aliondolewa uwanjani baada ya kucheza dakika 19 pekee. Aliumia mgongoni.

Mzaliwa huyo wa Conakry, Guinea alipokea matibabu uwanjani kwanza kabla ya kuondolewa na kupelekwa hospitalini. Kwa mujibu wa tovuti ya klabu hiyo, Keita “alifanyiwa uchunguzi wa kimatibabu wa tahadhari” kubaini hali yake.

Hakuna taarifa zozote kuhusu ni lini nyota huyo mwenye miaka 23 anatarajiwa kuondoka hospitalini. Keita amewachezea Liverpool mechi tisa msimu huu, ikiwa ni pamoja na kuanza mechi nne Ligi ya Premia.Alikuwa anawachezea mara ya kwanza katika Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya. Keita ni mchezaji mwenye miguu yenye kasi, ni mchezaji ambaye makocha wengi wangependa kuwa naye.

Keita ana nguvu na akili ya kuwapangua na pia kuwapiga chenga wapinzani na kisha maono ya kuweza kufanikisha mashambulizi na kufunga mabao au kusaidia kuyafunga.

Mkufunzi wake katika klabu ya Leipzig Ralph Hasenhutt wakati mmoja alimtaja kuwa kiungo muhimu kwa kipaji chake kisichokuwa cha kawaida. Nyota huyo aliyezaliwa mjini Conakry aliwavutia wengi na kuilazimu Liverpool kuweka uhamisho uliovunja rekodi kwa wachezaji wa kutoka barani Afrika wa £48m ili kupata huduma zake kuanzia mwezi Julai 2018. Huku Leipzig wakisema kuwa wasingemuuza bali ni kulingana na sheria ya uhamisho.

Matokeo ya mechi za Jumatano UEFA

  • PSG 6-1 Red Star Belgrade
  • Lokomotiv Moscow 0-1 Schalke
  • Atl Madrid 3-1 Club Brugge
  • Tottenham 2-4 Barcelona
  • Napoli 1-0 Liverpool
  • Borussia Dortmund 3-0 Monaco
  • PSV Eindhoven 1-2 Inter Milan
  • FC Porto 1-0 Galatasaray

Chanzo BBC

By Ally Juma

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents