Michezo
Liverpool yakamilisha usajili wa beki wa Southampton, Nathaniel Clyne kwa dau la Pauni Milioni 12.5
Timu ya Liverpool imemsajili Nathaniel Clyne, kutoka Southampton kwa pauni milioni 12.5. Mchezaji huyo beki wa pembeni mwenye umri wa miaka 24, amesaini mkataba wa miaka mitano na anakuwa mchezaji wa sita mpya kusajiliwa kuelekea msimu ujao.