Habari

Mabaki ya ndege ya EgyptAir yabainika yalipo

Mamlaka ya Misri imesema mabaki ya ndege ya EgyptAir ambayo ilianguka katika bahari ya Mediteranian mwezi uliopita ikiwa imebeba abiria sitini na sita yameweza kubainika yalipo.

160521031956_egyptair_airbus_320_512x288_reuters_nocredit

Katika maelezo yaliyotolewa na kamati husika ya uchunguzi wa ajali hiyo wanasema ,meli inayotafuta mabaki ya ndege ya EgyptAir imeweza kubaini maeneo kadhaa ambayo mabaki ya ndege ya A320 yapo na kutoa picha ya kwanza ya masalio hayo.

Kwa sasa kikosi hicho cha wakaguzi walioko melini watachora ramani wakionesha vielelezo vya mabaki ya ndege yalivyoeneo. Ndege hiyo iliyopotea baada ya kutoonekana kwenye rada wakati ikiwa inatokea Paris kuelekea Cairo. Huku ikiwa inadhaniwa kuwa lilishambuliwa na bomu.Lakini hakuna kikosi chochote cha kigaidi kilichodai kuhusika na kuangusha ndege hiyo.

Source: BBC

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents