Burudani

Bongo ikijua uwezo wangu ndio nitatoa collabo zangu na wasanii wa nje – Galaxy

Msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Galaxy amesema kuwa hataki kuachia collabo zake alizofanya na wasanii wa nje kwa sasa mpaka mashabiki watakapotambua uwezo wake vizuri.

12383209_646788105460940_1016128086_n

Mpaka sasa inadaiwa kuwa Galaxy tayari kashafanya collabo na msanii wa Zambia, Roberto huku wakiwa kwenye maongezi na menejimenti ya Patoraking ili wafanye kazi msanii huyo wa Nigeria.

Akiongea na Bongo5, Galaxy amesema, “Sidhani kama kufanya kazi na msanii wa nje ndiyo kutoka, hapana wapo wengi sana wamefanya collabo na wasanii wa nje lakini bado wapo kawaida tu.”

“Onyesha kwanza uwezo wako na unapokuwa unafanya collabo na wasanii wa nje tayari unakuwa umeshajitengenezea. Mimi nina connection na wasanii wan je na kuna wengine ninatakiwa kufanya nao kazi na kuna wengine ambao tayari nimeshafanya nao kazi,” aliongeza.

“Lakini siwezi kuachia kazi niliyofanya kazi na msanii aliyenizidi kwa sasa hivi, mpaka mashabiki wangu watambue vizuri uwezo wangu ndiyo nitaachia hizo kazi nyingine,” alisema.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents