Tupo Nawe

Mad Ice atoka na ‘TE AMO’

mad_ice

Msanii wa siku nyingi wa miondoko ya R&B na pop MAD ICE, amerudi upya kimuziki baada ya kuachia pini mpya inayokwenda kwa jina la TE AMO.

Msanii huyo mzaliwa wa Uganda ambaye kwa muda mrefu alikuwa akifanya shughuli zake za kimuziki nchini Tanzania, kwa sasa amehamisha makazi yake jijini Helsinki nchini Finland.

Nyimbo hiyo ambayo imetengenezwa katika studio za Finnvox imefanyiwa kazi na produsa mkongwe Oona Kapari pamoja na Mad Ice mwenyewe sambamba na bendi yake.

Nyimbo hiyo ni muendelezo wa kazi zake mpya ambazo zitajumuishwa kwenye albamu yake mpya itakayoitwa “Maisha EP” inayotarajiwa kutoka rasmi mwezi wa 4 mwakani.

Baadhi ya nyimbo ambazo zitakuwemo kwenye albamu hiyo ya Mad Ice ni pamoja na Nisikilize, Mapenzi  na nyimbo nsumu.

Bofya hapa kusikiliza wimbo huo sasa hivi!

Tayari video ya wimbo huo TE AMO imesharekodiwa na Charlie Harjulin, bofya hapa kusikiliza wimbo na hapa kuangalia  na utaiona hapa hapa bongo5.com

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW