Burudani

Madee amtaja ni mchezaji yupi mkali kati ya Ronaldo na Messi

Licha ya kufanya muziki, muimbaji wa ‘Vuvula’ Madee ni shabiki mzuri wa soka.

Madee

Hivi karibuni Madee alikuwa akiongea na kipindi cha Sports Xtra cha Clouds FM na aliulizwa na Shaffih Dauda kuwa yeye ni shabiki wa mchezaji gani kati ya Cristiano Ronaldo na Lionel Messi na nani mchezaji mkali kati yao.

“Messi amecheza Barcelona kwa muda mrefu na amekuwa bora kwa pale na tunakubali,” alijibu.

“Lakini mchezaji mkali lazima aweze kufanya vizuri akiwa na wachezaji tofauti kwenye mazingira tofauti na timu tofauti kwa mawazo yangu. Mimi nimemuona Ronaldo akiwa kwenye level ya juu akiwa Manchester na Real Madrid. Lakini Messi sijui kama akiwa Manchester atakuwa na kiwango kile kile? Ssasa mimi namkubali Ronaldo japokua Messi na yeye mkali.”

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents