Burudani

Suma Mnazaleti awekwa kitomoto kwa kukejeli ujumbe wa Mabeste, aomba radhi

Rapper Suma Mnazaleti yupo kwenye kitimoto. Ni baada ya kuandika maneno ya kukejeli ujumbe wa Mabeste aliyeomba kusaidiwa na mashabiki na wadau wa muziki ili aweze kumtibu mke wake.

c4d0dfa4294611e3b03722000a1fc75a_7

Suma alitoa maoni hayo chini kwenye picha katika post ya Mabeste:

11078483_1689797191247752_878030102_n

Kauli hiyo iliwakasirisha watu wengi walioanza kumshambulia kwa matusi mazito.

Hata hivyo rapper huyo amelazimika kuomba radhi kwa kudai kuwa sisi yeye aliyeandika maneno hayo bali ni mmoja kati ya watu aliowahi kusimamia akaunti yake aliyeamua kumfanyia hujuma!!!

“4 YEARS AGO MI NA @mabeste_tanzania KATIKA MOJA YA NYIMBO ZANGU TAFAKARI. NACHUKUA NAFASI HII KUMUOMBA RADHI @mabeste_tanzania na MKEWE @lisa_fickenscher NA WATANZANIA WOTE KWA UJUMLA-KUTOKANA NA COMENT ILIYOTOKA KUPITIA AKAUNTI YANGU HII YA INSTAGRAM KWENDA KWNYE POST YAKE ALIYOPOST JANA YA KUHITAJI MSAADA WA KUMUUGUZA MKEWE,” ameandika.

“IMENIWEKA KWENYE WAKAT MGUMU BAADA YA KUGUNDUA ILO JIONI YA JANA CM NYINGI MSG NYINGI ZILIFIKIA, LAKINI KWA SABABU SIKUWA NA SMARTPHONE CKUWEZA KUPOST CHOCHOTE. TWENDE KWENYE KILICHOTOKEA– MI NDO KIJANA PEKEE AMBAE TOKEA NIPOTEZE SMARTPHONE CJANUNUA TENA NA NATUMIA NOKIA YA TOCHI. BAADHI YA MAPROMOTA, WASANII NA BAADHI YA DJS WALIOKUTANA NA MIMI HVI KARIBUNI NA WATU WOTE WANAONIZUNGUKA WANAJUA KUWA SINA SMARTPHONE. LAKINI KUTOKANA NA UMUHIMU WA SOCIAL NETWORK KWA DUNIA YA SASA ILI KUFIKISHA HABARI ZANGU ZOZOTE NILITEUA WATU WAWILI NA NIKAWAPA AKAUNTI ZANGU NA PASWORD. FACEBOOK, INSTA NA TWITTER PIA ILI WAWE WANAZIENDESHA WAO NNAPOKUWA NA LOLOTE LILE NAWAJUZA NA NNAENDELEA KUWA UPDATE.. NA MMOJA MUDA MWINGINE UWA MPAKA NASAFIRI NAE. POST YA NDUGU YANGU RAFIKI WA KARIBU WA MIAKA MINGI TUSHAFANYA MPAKA KAZI PAMOJA AUDIO VIDEO SHOWZ KUKESHA PAMOJA @mabeste_tanzania mpaka interview kama jiwe la week kwa @bdozen naenda nae gym dah.. ICNGEFIKIA HUKO ATA KAMA NA ROHO MBAYA SIO YA KIAC ICHO.. MMOJA KATI YA WATU AMBAO WALIKUWA WANA RUN AKAUNT ZANGU NDIYE ALIYEFANYA KITENDO ICHO CHA KUCOMENT UMAKU KWNYE POST YA MABESTE.. NAOMBA RADHI WATANZANIA, NAMUOMBA RADHI MABESTE NA MKEWE,” ameongeza.

“NAOMBA RADHI MASHABIKI WA MZIKI WA TANZANIA KWA TATIZO LILOTOKEA NAOMBA RADHI MEDIA ZOTE.. ALIYENIFANYA NIONEKANE MPUMBAVU KASHAFANIKIWA.. KAMA MATUSI NIMEPATA YA AINA ZOTE CDHANI KAMA KUNA LILILOBAKI- NAMALIZA KWA KUSEMA AKAUNT ZANGU ZOTE ZIMERUDI MIKONONI MWANGU NA NTAZIENDESHA MWENYEWE BUDAA @mabeste_tanzania @lisa_fickescher NAOMBENI MSAMAHA WENU.”

Suma hajaishia hapo kwani kwenye profile ya akaunti yake ya Instagram pia ameandika: BUDAA NAOMBA RADHI MWANANGU @mabeste_tanzania MATUSI YAACHE YAENDELEE ILA UNAJUA MI NA WEWE TUNAVYOISHI- MTU WA KARIBU KA2MIKA KUNIUA MAADUI SHANGWE.”

Unaamini maneno ya Suma?

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents