Habari

Madrasa Baadae Muziki kwanza

20%Kufuatia suala zima la buku Abas Hamisi a.k.a 20% amemaliza shule ya msingi kimanzichana, hakubahatika kuendelea kupandisha vidato na badala yake akawa anafundisha elimu ya madrasa

Kufuatia suala zima la buku Abas Hamisi a.k.a 20% amemaliza shule ya msingi kimanzichana, hakubahatika kuendelea kupandisha vidato na badala yake akawa anafundisha elimu ya madrasa huko maeneo ya kimanzichana.


“Ni hisia zangu ndizo zilizonishawishi nikaingia kwenye masuala ya muziki hakuna msanii yeyote aliyanihamasisha kufanya muziki” alisema 20%”


Akielezea sababu zilizomfanya ajiite 20% alisema “nilikata tamaa nilipooana kila mbinu ninayoitumia ili nitoke nabuma, hivyo matumaini yaliyobaki niliweza kuyakisia kuwa ni kama asilimia 20, ghafla nikatoka nikaona hili ndio jina la kuchomoka nalo.


Ali weza kurekodi ngoma 14 kabla hata hajatoka na katika kipindi chote hicho alikuwa akitest zali lakini hakuwa akitusua na mpaka ngoma yake inabamba yeye hakuwa na habari kabisa alikuwa akiendelea na michongo yake huko Kimanzichana.


Kama zali songi lake ‘money money’ likabamba, na baada ya hapo mtu mzima akatupa jiwe lingine hewani ‘binti kamanzi’ hapo ndio wadau walipoanza kumtolea macho, fasta fasta akakamilisha albam na kuitupa sokoni ambapo inafanya vizuri ile mbaya.


Baada ya kijana 20% kutoka aliachana na mitkasi za kufundisha madrasa “unajua hata mtaani wazee na maustaadh walionekana kukerwa na maamuzi yangu, sikujali kwani niliamini watazoea tu na kweli wamezoea mpaka leo napeta tu”-20%


20%

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents